Jumamosi , 7th Jun , 2025

Rapper Mr Blue amefunguka kuwa yeye ni moja ya wasanii wachache bongo ambao inawezekana akawa na ngoma nyingi zaidi na wasani wachanga zaidii, Blue amesema hayo siku za hivi karibuni alipokuwa akifanya mahojiano na waandishi wa habari

Pichani ni Mr Blue

 

"Wepesi wa kufanya kazi na mimi upo mkubwa kama kuchana karatasi tu au kuzima Tv mimi nina kolabo sio chini ya 200 za wasanii wachanga na ilo swala bado linaendelea kama unataka kushirikiana na mimi'' Amesema Mr Blue

"Siangalii hela sana na naangalia hela sana na yote nafanya unaweza ukaja na nidhamu tu na tukafanya wimbo hata kama huna kipaji kwasababu nishawahi kuimba na watu wa aina hiyo na baadae wakaja kuwa wasanii wakubwa'' Amesema Mr Blue

"Na wale wenye vipaji kabisa naimba nao na hata hao wenye hela na hawana kipaji pia nawakaribisha'' Amesema Mr Blue