"Nina pea 300 za viatu" – TID

Jumamosi , 27th Apr , 2019

Msanii wa muziki wa Bongo Fleva, TID, ameweka wazi kuwa yeye kama msanii anaishi kwa kujibrand, na ndiyo sababu inayomfanya awe na vitu vingi ikiwemo mavazi.

Akizungumza na JR Junior katika Bongo Fleva Top 20 ya East Africa Radio, TID amesema kwamba miongoni mwa vitu hivyo ni nguo nyingi ambazo hawezi rudia kwa mwezi nzima, na pea za viatu zaidi ya mia tatu (300).

Soma alichofunguka TID  

“Mimi kabati langu baba labda zije fuso mbili, I have a very big wardrobe ya nguo, nikiamua kuvaa kuanzia monday ya mwezi wa 3 nitavaa mpaka monday nyingine ya mwezi wa 4  sirudii, na viatu  ninavyo 'like three hundred pair of shoes', mpaka mama ananiambia huoni kama vurugu, vitoe hivi, to me fashion ndio kitu kinaniweka hai, kinanipa brand kinaniweka hai, nimeleta revolution watu wamekuwa wasafi sasa hivi”, amesema TID.

TID amekuwa ni mmoja ya wasanii ambao waliutoa muziki wa Bongo Fleva na kuupeleka kimataifa miaka ya 2000, wakati muziki huo unaanza kutambulika.