Jumamosi , 27th Apr , 2019

Imezoeleka kuwa wanawake pekee ndiyo wameumbiwa kuingia period kila mwezi mara pale wanapovunja ungo, kudhihirisha kuwa sasa wako tayari kuweza kubeba ujauzito na kuzaa

Lakini ni kitu cha ajabu kusikia kuwa hali hiyo hutokea kwa mwanaume. Nikujuze tu kuanzia sasa unatakiwa ufahamu kuwa hata wanaume wanaingia hedhi, lakini sio kama ile ya wanawake ambapo wao hutoka damu sehemu zake za siri (baada ya yai kutorutubishwa na kutoka).

Jinsi wanaume wanavyopata hedhi

Kwa wanaume kitendo hiki huwa tofauti kabisa. Kwa mujibu wa mtaalamu wa psychotherapist na mwandishi wa kitabu cha Male Syndrome (IMS), Jed Diamond, PhD. Diamond, amedhirisha hili na kusema kwamba wanaume nao huingia period lakini ni tofauti na ile ya wanawake.

Kwa wanaume wao hukutana na mabadiliko ya homoni za testosterone ambazo husababisha mabadiliko ya kiafya, ikiwemo kuwa na msongo wa mawazo, uchovu na kubadilika kwa hali kila mara.

Hali hii pia huwatokea wanawake pale wanapoingia hedhi na muda mwingine huwaletea maumivu makali ya tumbo kutokana na mabadiliko ya mwili katika via vyake vya uzazi, lakini kwa wanaume haina madhara makubwa na wala hawawezi kupata damu kama wanawake, zaidi ya kuhisi mabadiliko kutokana na kutotulia kwa homoni.

Source: Health Line