Jumanne , 29th Dec , 2020

Msanii wa HipHop na mwanaharakati wa masuala ya kijamii Kala Jerermiah, amesema ana mpango wa kuingia Bungeni mwaka 2025 ila atatumia nafasi hiyo ili baadaye aje kuwa kiongozi wa Nchi yaani Rais.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimvalisha kofia msanii wa HipHop Kala Jeremiah

Akizungumzia hilo kupitia kipinmdi cha Planet Bongo ya East Africa Radio Kala Jeremiah amesema kuwa 

"2025 itakuwa muda mzuri na nitakuwa nimejipanga lakini nitaingia kwenye Ubunge kama njia tu kwa sababu siutamani sana Ubunge kikubwa ambacho nakitamani ni kuwa kiongozi wa Nchi  Mheshimiwa Jeremiah Kala Masanja halafu hata jina pia limekaa"

Aidha Kala Jeremiah ameendelea kusema anahimiza watanzania waendelee kupenda vitu vyao kwa sababu hakuna mtu ambaye anayeweza kuwasaidia kama hawatopenda vitu vyao. 

Zaidi tazama hapa chini kwenye video