Jumamosi , 22nd Aug , 2015

Nyota wa muziki ambaye pia ni mkufunzi na msakata dansi mahiri akiwa vilevile ni Jaji wa Mashindano ya Dance 100% 2015, ameweka wazi kuwa kwa sasa yupo katika hatua za mwisho za uandikishaji wa taasisi hiyo tayari kwa kuanza kazi hivi karibuni.

Super Nyamwela

Kauli hii ya Super Nyamwela, inakuja baada ya kutangaza mpango wake mkubwa wa kuiendeleza tasnia ya dansi hapa nchini kwa kufungua chuo cha madansa, nia hasa ikiwa ni kuacha alama ya mchango wake hasa baada ya kuitumikia tasnia hiyo kwa miaka mingi na binafsi kujivunia mafanikio makubwa.

Nyamwela ameieleza eNewz kuwa, utaratibu maalum wa wale wote wenye ndoto za kujiendeleza kupitia dansi utawekwa wazi hivi karibuni kwa gharama ambazo watazimudu, lengo lake hasa likiwa ni kuipeleka mbali zaidi fani hiyo ambayo inaendelea kufunguka kimataifa.