Ommy Dimpoz adai kujipanga kwa Ali Kiba

Ijumaa , 29th Nov , 2019

EATV & EA Radio Digital, imepiga stori na msanii na boss wa lebo ya pozi kwa pozi (PKP), Ommy Dimpoz, ambaye amesema amejipanga vyema ili kuendana na ziara ya kimuziki ya rafiki yake Ali Kiba, iitwayo AliKibaUnforgettable Tour.

Wasanii wa muziki Bongo, Ommy Dimpoz na Ali Kiba.

Ommy Dimpoz ameeleza kuwa ziara hiyo ni ya kifamilia hivyo ni lazima awepo.

"Unajua hii ni 'Tour' ya kifamilia, naweza kusema hivyo, pia Ali Kiba ni mtu wangu, kwahiyo kuna tarehe ambazo nitakuwepo kweli kwenye show, naweza kusema nimejipanga pia nina msisimuko, nipo tayari kutoa msaada kwa ndugu yangu na nimejipanga" amesema Ommy Dimpoz.

Ziara hiyo ya kimuziki ya Ali Kiba, tayari imeshaanza mkoani Tabora, tangu walipowasili siku ya Jumatano ya Novemba 27, 2019,  ambapo watakuwa  pamoja na timu nzima ya East Africa Radio na East Africa Television.

Ndani ya ziara hiyo Ali Kiba atafanya shughuli za kijamii, kutembelea vyuoni, kutoa misaada kwa wagonjwa, kucheza mpira pamoja na show yenyewe itakayofanyika siku ya Jumamosi ya Novemba 30, katika viwanja vya Ali Hassan Mwinyi kuanzia saa 12 jioni.