Alhamisi , 16th Sep , 2021

Mchekeshaji Mr Bigibigi Pacha wa Mose Iyobo amesema wazo lake halikuwa kuiga sauti za mastaa bali ni kufanya mbwembwe wanazofanya mastaa mitandaoni kwa sababu wanapenda kiki.

Picha ya pacha wa Mose Iyobo

Mr Bigibigi anaendelea kusema katika kuonyesha uhalisia wa kitu ndiyo imempelekea kuuvaa uhusika wa mtu anayetaka kumuigizia sauti yake.

Mpaka sasa ameweza kuiga sauti za mastaa kama Mose Iyobo, Hemedy PHD, Shilole,na Haji Manara.