Jumatatu , 8th Feb , 2021

Ni 'headlines' za msanii wa filamu Othman Njaidi maarufu kama Patrick Kanumba ambaye ametoa 'comment' yake kuhusu kinachoendelea mitandaoni kati ya majibu aliyoyoyatoa Mama Kanumba kwa Elizabeth Michael kuhusu kifo cha mwanaye Steven Kanumba.

Kushoto ni Mama Kanumba na Elizabeth Michael, kulia ni Patrick Kanumba

Kupitia EATV & EA Radio Digital, Patrick Kanumba amesema ni kweli alikuwa mtu wa karibu na marehemu Steven Kanumba ila tayari mama yake mzazi ameshasema hivyo hawezi kumpinga na hawezi kuwa upande wowote.

"Mimi namjua Kanumba tu, nilikuwa mtu wake wa karibu na ananihusu, ila yule ndiyo mama wa marehemu na ameshamaliza kila kitu hivyo siwezi kupinga wala kuwa upande wowote kwa sababu ameshatangulia hivyo tuendelee kumuenzi marehemu" amesema Patrick Kanumba 

Zaidi tazama hapa chini kwenye video.