Pilipili amfungukia 'x' wa mchumba wake

Jumatano , 9th Jan , 2019

Mchekeshaji maarufu bongo, Emmanuel Mathias 'MC Pilipili' ambaye hivi karibuni amemvisha pete mchumba wake, amefunguka juu ya tuhuma zinazodaiwa kuwa ametumia pesa kumpata mwanamke huyo kutoka kwa mwanaume wake wa zamani.

Akizungumza na www.eatv.tv, MC Pilipili amesema kwamba anamuhurumia kijana huyo, lakini anaamini atapata mwanamke mwengine kwani wanawake ni wengi Tanzania.

Aisee nampa pole,  Tanzania inaonesha wanawake ni wengi kuliko wanaume, kwa hiyo sio rahisi kwa yeye kutembea na mwanaume mwingine, lakini ni rahisi kupata mwanamke, atapata mwanamke mwingine, kwani wanawake ni wengi Tanzania na duniani”, amesema Mc Pilipili.

Ikumbukwe kwamba mwishoni mwa wiki iliyopita, Mc Pilipili amechumbia msichana mmoja anayejulikana kwa jina la Philomena Thadey maarufu kama 'Cute Mena', na baada ya muda mfupi zikaibuka tuhuma mitandaoni kuwa alikuwa mchumba wa mwanaume mwingine hapo kabla.