Ijumaa , 19th Nov , 2021

Msanii wa Bongo Fleva na aliyewahi kuwa mbunge wa Mikumi Joseph Haule maarufu kama ProfessorJay, amesema anashangaa kwanini BASATA wanakuwa wakali tu kwenye nyimbo za siasa na sio zile zinazoimba lugha isiyo nzuri yenye kuzungumzia zaidi vitendo vya mapenzi.

ProfessorJay

Kauli hiyo ameito hii leo Novemba 19, 2021, kwenye kipindi cha SupaBreakfast cha East Africa Radio na kusema kwamba kuna baadhi ya nyimbo za mapenzi zinazoimbwa siku hizi hawezi kuzisikiliza akiwa na mtoto wake.

"Nashangaa BASATA wanakuwa wakali sana kwenye mambo ya siasa lakini kwenye haya mambo ya mapenzi wakija kusikiliza na kuchambua lugha ni ngumu sana huwezi kuzisikiliza, lakini wasanii wanakuambia wanafanya vile sababu ni biashara na watu wanapenda, no lazima tu-balance ili kutengeneza kizazi chenye nidhamu kama ambavyo sisi tulitengeneza," amesema ProfessorJay