Rachel afunguka yaliyomkuta alipokwenda Uarabuni

Jumatano , 14th Feb , 2018

Msanii wa muziki bongo Rachel maarufu kama Rachel Kizunguzungu, amefunguka juu ya sakata lake la kwenda nchi za Uarabuni na kukutwa na mabalaa, ikiwemo kutumia madawa ya kulevya na kutelekezwa huko na mwanaume aliyekwenda naye.

Akizungumza kwenye Planet Bongo ya East Africa Radio, Rachel amesema ni kweli alikwenda Arabuni kwani ilikuwa ndoto yake tangu utotoni, na alipokwenda hukomilikuwa ni kutimiza ndoto zake na kuamua kubaki kwa muda kula raha.

“Kweli nilienda na nilienda na kazi zangu sio kwa ajili ya mapenzi, nakuhusu kubaki kule kule sikutamani, lakini ndoto zangu tangu niko shule ilikuwa kufika kwenye nchi za Arabuni, nikasema kwa nini nisikae hata miezi miwili mitatu tuienjoy! Nilikuwa na mpenzi wangu ambaye ni mwarabu, na nilipokuwa kule nilikaa mwenyewe, sikupokonywa passport na wala sikuzidisha muda wa kukaa, nilikuwa nimekaa mwenyewe kwa raha zangu na mtu wangu, hizo stori ni watu tu kujiongeza”, amesema Rachel.

Rachel amesema hata taarifa za yeye kuwa kwenye hali mbaya akitumia madawa ya kulevya hazina ukweli, hivyo watu wasiamini maneno wanayoyasikia kwa watu.