Jumatano , 13th Mei , 2015

Wasanii mahiri wa nchini Uganda, Radio na Weasel wameingia katika mapambano na muandaaji matamasha maarufu kwa jina la promota Baalam.

Wasanii nyota wa nchini Uganda, Radio na Weasel

Chanzo cha ugomvi wao kimetajwa kuwa ni wasanii hao kutokutokea katika onesho ambalo tayari walikuwa wamelipwa kiasi cha shilingi milioni 7 kulifanya huko Gulu.

Kufuatia kitendo hicho ambacho Baalam alikiripoti polisi, Meneja wa wasanii hao Labeja Lawrence alijikuta akiwekwa chini ya ulinzi wakati kundi hili likiwa katika mchakato wa kufanya onesho lingine hivi karibuni, kitendo ambacho wamekichukulia kama mkakati wa promota huyo kuwaharibia kazi yao.

Moze Radio amekuwa ni mtu wa kwanza kumtuhumu Baalam hadharani kwa kutaka kuwaharibia shoo, kauli ambayo promota huyo amekasirishwa nayo na kuahidi kumfundisha msanii huyo somo.