Ijumaa , 21st Oct , 2016

Label ya Muziki ya Rose Ndauka imetambulishwa baada ya uzinduzi wake jijini Dar es Salaam sambamba na kumtambulisha msanii wake wa kwanza wa kizazi kipya aitwaye Casso.

Rose Ndauka (Kushoto) akiwa na Casso

Akizungumza na waandishi wa habari staa huyo wa filamu aliyeingia kwenye tasnia ya muziki Rose Ndauka amesema amefurahia kuzindua Label yake hiyo ambayo ni ndoto yake ya muda mrefu hasa katika kusaidia vijana katika kazi za muziki

“Siwezi eleza najisikiaje, nimetimiza ndoto yangu ya muda mrefu na hii inachangiwa na mafanikio yangu kwenye filamu hivyo ni shauku yangu kwamba vijana watanufaika hasa wanamuziki” amesema

Rose Ndauka amesema, "Kwenye label yangu hii mpya tuna wasanii watatu ila kwa leo tunamtambulisha kwenu Casso ambaye leo pia kwa mara ya kwanza ataachia video ya single yake mpya iitwayo Kitonga.wimbo ukiwa umetayarishwa na producer Man Water"

Ndauka ameomba mashabiki wake na mashabiki wa muziki wa Bongo Fleva kumsapoti Casso na kusapoti Label ya Ndauka Music ambayo inalenga kukuza kazi za sanaa.