"Rose Ndauka bado sana kuimba" - Shamsa Ford

Jumatano , 21st Apr , 2021

Msanii wa filamu Shamsa Ford amemchana ukweli rafiki yake Rose Ndauka baada ya kuingia kwenye muziki kwa kumwambia hajui kuimba bora waaendelee kuigiza filamu huko kwengine waachie wasanii kama Maua Sama na Rosa Ree.

Kushoto pichani ni Shamsa Ford, kulia Rose Ndauka

Shamsa Ford amesema yeye binafsi hajui kuimba ila anapenda kucheza na kwa upande wa Rose Ndauka bado sana ila anasubiria show yake ambayo atakuwa anamuangalia na kumsikiliza huku akiwa ameshika shavu.

"Rose Ndauka anapenda kuimba sio kwamba hajui, anamuelekeo kidogo na muda utaongea zaidi ila kwangu mimi naona bado kabisa anisamehe kwa hili bora tuendelee kufanya 'movie', mpaka huu mwaka uishe tutaona mengi muziki tuwaachie wakina Maua Sama, Nandy na Rosa Ree" amesema Shamsa Ford 

Zaidi mtazame hapa chini kwenye video.