Alhamisi , 2nd Apr , 2020

Staa wa kike wa muziki wa BongoFleva Vanessa Mdee, amefunguka suala lake la kukaa kimya kwa muda mrefu, baada ya kuingia katika mapenzi na msanii wa filamu na muziki Rotimi.

Vanessa Mdee na Rotimi

Sasa kupitia video aliyopost katika mtandao wa Instagram, Vanessa Mdee akieleza sababu za kuwa kimya kwa muda mrefu, akatokea mpenzi wake Rotimi na kusema maneno ya kwamba "Hatuachani, Hatuachani"

"Mambo vipi natumaini kila mtu anajilinda kwa ugonjwa wa Corona kwa kipindi hiki , nimekuwa kwenye soko kwa muda wa miaka 13 bila kuchukua mapumziko, nimefanya vile ambavyo Vee anatakiwa kufanya, nimetulia, nimetafuta upendo mzuri, nina furaha na ninafurahia kula maisha" amesema Vanessa Mdee.

Aidha kupitia video hiyo ameeongeza kusema "Napenda kuwashukuru kwa kuendelea kunisapoti na mapenzi yenu mnayonionesha, nataka kuwashauri kuwa tafuta muda wako mwenyewe hasa kwa kipindi hiki cha ugonjwa, omba sana, kuwa na mawasiliano na Mungu, kuwa makini na familia yako na mmoja unayempenda".