
Baada ya kesi kuendeshwa kwa muda mrefu katika mahakama za Marekani, hukumu rasmi imetolewa dhidi ya msanii Sean Kingston na mama yake mzazi, ambapo wote wawili wamepatikana na hatia ya kushiriki katika njama ya utapeli wa kutumia mtandao kwa nia ya kujinufaisha kifedha.
Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na vyombo vya sheria, Sean Kingston na mama yake walihusika katika visa kadhaa vya kuwasilisha risiti za kughushi kwa kampuni mbalimbali, wakidai kuwa wamelipia bidhaa wakati ukweli ni kuwa hawakufanya malipo yoyote.
Makampuni Yaliyoathirika ni pamoja na:Kampuni ya magari ya kifahari aina ya Escalade,Kampuni ya kuuza saa za bei ghali,Kampuni ya kuuza runinga (TV) za hali ya juu,Walikusudia kupata bidhaa hizo kwa njia ya udanganyifu, kwa kutumia vielelezo feki vya malipo.
Sean Kingston: Miaka 3 na miezi 5 jela,Mama yake mzazi: Miaka 5 jela,Mahakama imeeleza kuwa makosa haya ni ya kiwango kikubwa, na yalifanyika kwa mpangilio wa kitaalamu kwa lengo la kudanganya kampuni kadhaa na kujipatia bidhaa bila malipo halali.