Jumatatu , 26th Mei , 2014

Polisi nchini Kenya wanachunguza tukio la ugomvi baina ya Seneta wa Nairobi Mike Mbuvi Sonko na Mbunge Mwakilishi wa Wanawake Rachael Shebesh, uliotokea kwenye klabu moja ya usiku, siku ya jumamosi.

Mike Sonko

Kwa mujibu wa Sonko ambaye ni maarufu kwa mavazi ya kisasa na swagga za vijana anadai kuwa gari lake la kifahari aina ya Range Rover lenye thamani ya shilingi milioni 8 za Kenya ndio chanzo cha ugomvi uliopelekea kufyatuliana risasi.

Hata hivyo taarifa nyingine zimedai kuwa Shabesh alimfuata Seneta Sonko, na kumuuliza kwanini anamfuata fuata, hii ni baada ya Sonko na kundi lake la watu 30 kuwasilia kwenye Klabu hiyo saa moja usiku na kumkuta Shebesh akiwa ndani na wafuasi wake.

Wakati hayo yakijiri picha zinazomuonyesha Seneta Soko na Mbunge Shebesh wakiwa wamekaa katika pozi linaloashiria kuwa na uhusiano wa karibu mno zimekuwa zikisambwazwa kwenye vyombo vya habari.