
Seyi Shay ametoa kauli hiyo kwenye mahojiano maalum katika kipindi cha DADAZ cha East Africa Television, wakati akieleza sababu ya wasanii wa Nigeria wengi wao kuonekana kwenye albam ya Beyonce na si wasanii wa Afrika Mashariki.
"Sababu pekee iliyotufanya muziki wa Nigeria na wasanii wetu, kushiriki kwenye albamu ya Beyonce tunatumia nguvu sana kuutangaza muziki wetu na ukisikiliza sisi muziki wetu una ladha ambayo ni ya kikwetu kikwetu." amesema Seyi Shay.
Aidha Seyi Shay amezungumzia mahusiano yake na msanii wa Bongo Fleva Ommy Dimpoz, na kusema kuwa walijuana nchini Kenya na hapo ndipo walipofanya wimbo wa pamoja uitwao Yanje.
"Kuhusu kukutana na Ommy Dimpoz kwanza naupenda sana muziki wake, lakini pia alishakutana na PR wangu kule Kenya kisha akanikutanisha naye akaniambia Ommy Dimpoz kazipenda nyimbo zangu hapo ndipo tulijuana." amesema