Ijumaa , 10th Oct , 2014

Kutokana na mahadhi ya muziki wa kizazi kipya kwa sasa kuelekea sana katika vionjo vya Afrika Magharibi, mtayarishaji muziki Sheddy Clever alifunguka kuwa wasanii wenyewe ndio wanachangia katika hilo ingawa yeye huwashauri kufanya tofauti.

mtayarishaji wa muziki nchini Tanzania Sheddy Clever

Sheddy amesema kuwa, kwa nafasi yake huwa anashauri wasanii hawa kutumia ubunifu wa kwetu zaidi ingawa saa nyingine anabanwa na misingi ya kibiashara kulingana na mahitaji ya msanii husika ambaye anafanya naye kazi.