Jumatano , 25th Mar , 2015

Mtayarishaji Sheddy Clever, ameweka wazi mabadiliko ya mfumo wa kufanya kwake kazi kwa sasa baada ya kusimama kama mtayarishaji muziki mpya, na kusema kuwa katika kipindi hiki, project anazokuwa anafanya na msanii zinakuwa zina mikataba.

mtayarishaji wa muziki nchini Sheddy Clever

Sheddy amesema kuwa, kwa sasa anaona maslahi na mafanikio yanaonekana kwa upande wake tofauti na hapo awali ambapo alikuwa akiwaalika wasanii studio kwake na kufanya nao rekodi bure kwa malengo ya kujitengenezea nafasi yake.

Kauli hii ya Sheddy inakuja wakati huu ambapo bado mjadala mkubwa unaendelea juu ya uhalali wa maslahi ya watayarishaji muziki, ikilinganishwa na faida kubwa ambazo wasanii wanapata kutoka rekodi amabazo wametengeneza.