Jumanne , 29th Dec , 2020

Ni 'headlines' za burudani ambapo kutoka jamhuri ya watu wa mtandao wa Instagram imetawala stori ya vichambo kutoka kwa mwanamitandao Mange Kimambi na msanii na mfanyabiashara Zuwena Mohamed maarufu kama Shilole.

Kushoto ni msanii Shilole na kulia ni Mange Kimambi

Kichambo hicho kilianzishwa na Mange Kimambi ambapo amemchana Shilole kwa kuandika kuwa 

"Hivi Shilole my dear, hivi kwani ni lazima uolewe jamani unanisikitisha utatumika na hivi vitoto mpaka lini, hizo hela za kuwalea hao vijana wenye mama zao si uwawekee wanao 'savings bank' jamani, hivi Bongo ndiyo tuseme wanaume hakuna kabisa, wanamke mzuri mwenye shughuli zake kama Shilole anakosa kabisa mwanaume wa maana hadi inabidi alee kimtu ili akiite mume".

Baada ya muda Shilole naye akamjibu kupitia ukurasa wake wa Instagram kwa kueleza 

"Kuna muda ukifika pesa si kila kitu ila furaha ya mtu binafsi huja mbele mimi ni muumini mkubwa wa hiyo falsafa, tatzo la wanawake wengi bado wapo katika wapo katika desturi ya kuchuna ili waendelee kwa kutengemea vibabu dhambi hiyo iniepuke

"Penzi la kudandia ama kushea na mababa au vibabu vilivyooa siwez sio vitu vyangu 'and besides Romy ni above 30' tena mwenye shughuli zake kiuchumi..yeye sio hivyo mnavyomtasfiri, samahani dada yangu hayakuhusu" amejibu Shilole