Alhamisi , 16th Dec , 2021

Msanii na mfanyabiashara Zuwena Mohammed 'Shilole'  ameshea taarifa ya kupata ajali ya gari kwenye page yake ya Instagram akiwa maeneo ya Chalinze mkoani Pwani.

Picha ya msanii Shilole na gari alilopata nalo ajali

Katika video Shilole ameshukuru mungu kwa kuandika  "Mungu ni mwaminfu siku zote, Asante tumetoka salama"

Baada ya taarifa hiyo mastaa mbalimbali nchini na mashabiki wake wamempa pole Shilole kwa tukio hilo la kupata ajali.