Jumapili , 14th Jan , 2024

Msanii na Mwanasiasa maarufu Kenya Jaguar amesema hajawahi kunywa pombe, kuvuta sigara na bangi kwenye maisha yake yote.

Picha ya Jaguar

“Mimi sijawahi weka pombe kwa mdomo wangu, sijawahi kuvuta sigara na kuvuta bangi. Nawaambia hawa wasanii wakati wanaingia ukiitwa kwa show ukisema uwekewe Champagne 10 kuna wakati utakosa na utakunywa Chrome” amesema Jaguar

Pia amewashauri wasanii wa Kenya kama hawajajipanga kimuziki wasiwaambie watu wawachangie.