Jumanne , 1st Oct , 2019

Mshindi wa taji la ulimbwende kwa mwaka 2019/2020 hapa nchini Sylvia Sebastian, ametangaza kuwa yupo 'single' na kwamba hajaona msanii wala kigogo yoyote, ambaye atamshawishi kuingia naye katika mahusiano.

Miss Tanzania 2019, Sylvia Sebastian

Akipiga stori na EATV & EA Radio Digital, mlimbwende huyo amesema kuwa suala la mahusiano kwa sasa hajalipa kipaumbele na kwamba analinda kauli mbiu ya Miss Tanzania inayosema 'Urembo ni heshima'.

"Sina kigogo yeyote kwenye mahusiano, pia napenda mziki, lakini  bado sijajua ni msanii gani nampenda sana na kumfikiria kuwa naye kwenye mahusiano, sidhani kama yupo kwa sasa ila mimi namtaka mwanaume yeyote atakayeletwa na Mungu", amesema Sylvia.

Aidha Sylvia amemtaja Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Jokate Mwegelo kuwa ndiye mtu aliyemfanya kupenda masuala ya urembo.