Jay Dee aweka silaha zake hadharani

Tuesday , 12th Sep , 2017

Msanii mkongwe wa bongo fleva, Lady Jay Dee maarufu kama 'Komando Jide" amefunguka na kudai haoni sababu ya yeye kutoa wimbo mpya kila mara kwa madai nyimbo zake ni za hisia ambazo zinaweza kuishi miaka mingi.

Msanii mkongwe wa bongo fleva, Lady Jay Dee.

Jay Dee ameeleza hayo baada ya kuwepo wimbi kubwa la wasanii wakikimbizana kila uchao kutoa tungo mpya kwa mashabiki zao hata kama kazi ya awali haijakaa muda mrefu sokoni.

“Siwezi kutoa nyimbo mpya kila siku, kwa sababu nyimbo zangu ni za hisia, ambazo zinaweza kuishi hata miaka 10. Ni bora nitoe wimbo mmoja kwa mwaka lakini uwe unaishi miaka mingi kwa ladha ile ile siku zote," amesema Jay Dee.

Pamoja na hayo, Jay Dee amesema wasanii wengi wa kike wanashindwa kupambana katika muziki kutokana na kutopewa ushirikiano wa kutosha katika kile wanachokifanya japokuwa muda mwingine uongozi nao unachangia.

Lady Jay Dee ameachia ngoma ya 'I miss you' iliyotengenezwa na 'producer' Man water.