Jumanne , 9th Feb , 2021

Mara baada ya kuvunjika kwa ndoa yake ya pili, mkali wa muziki wa Dansi nchini Tanzania Charz Baba amesema sasa hivi hataki tena wanawake kwani anahisi wanamchezea na kumtenda kwenye mahusiano.

Charz Baba na mkewe siku ya ndoa yao

Charz Baba amesema bado anajiona ni kijana na hapendi mambo ya kihuni ndiyo maana ameweza kutulia mwaka mmoja bila ya kukutana na mwanamke kimwili 

"Mimi bado mvulana nina miaka 41 bado mdogo na sijakuwa, sasa hivi nina mwaka mmoja sijakutana na mwanamke kimwili, sitaki tena wanawake maana hawaridhiki naona wananichezea wananiacha sijui kwanini au labda nina kasoro gani, toka nianze kupambana kwenye ligi ya mapenzi napigwa mimi tu" ameeleza Charz Baba 

Zaidi mtazame hapa chini kwenye video.