
Wolper amefunguka hayo karibuni na kusema kwama kutokana na upendo wa kweli anaojitahidi kumuonyesha mwanaume anapokuwanaye kwenye uhusiano na kujikuta akiambulia maumivu, ameona bora aweke kando masuala ya mapenzi na kuwa`bize’ na kazi zake.
“Sina mpenzi kwa sasa nimeona bora niweke pembeni haya mambo nidili na kazi zangu tu ndo muhimu, nikisema nipende hawa wanaonisumbua `now’ nitapenda sana na nitakuwa kimapenzi, lakini bado wote wanaonisumbua hakuna aliyefaulu kunishawishi niwe naye,” alisema Wolper.
Wolper kwa sasa amekanusha kuwepo kwenye mahusiano baada ya kuachana na mpenzi wake ambaye ni mwanamuziki hivi karibuni