Jumatano , 17th Oct , 2018

Msanii wa Bongofleva, Snura amelamba shavu kutoka kwa msanii na mwandaaji wa muziki mkongwe nchini Marekani Snoop Dogg  baada ya nguli huyo kuweka video fupi ya wimbo wa Snura wa 'Zungusha' kwenye ukurasa wake wa Instgram.

Snura kushoto na Snoop Dogg kulia.

Ngoma hiyo ambayo video yake ilipandishwa kwenye mtandao wa Youtube Oktoba 1, 2017, ilijipatia umaarufu kwa watu mbalimbali kuicheza na kusambaza video zao mitandaoni na mwisho moja ya video hizo zimemfikia Snoop ambaye yupo nchini Zimbabwe kwenye shughuli zake maalum.

Baada ya kuona video yake imewekwa na Snoop Snura amepokea kwa furaha kitendo hicho na kuahidi kuendelea kufanya kazi nzuri ili mwisho wa siku dunia nzima imtambue.

Sikati tamaa ipo siku maajabu yangu yataifikia dunia, huu uswahili wangu kwa wenzetu ni burudani mpya na 'wanaenjoy' sana", amefunguka Snura.

Post ya Snoop Dogg

Snura pia ameusifu muziki wake na kusema  una asili ya uswahili na kamwe hatoacha kufanya uswahili wake kwani ndio unamtambulisha duniani.

Msanii huyo hivi sasa anatamba na ngoma yake mpya ya "Nani" aliyoiachia katikati ya mwezi uliopita.