Jumanne , 21st Jul , 2020

Mchekeshaji Idris Sultan amefunguka na kusema hataki kuwa mnafiki kwani Steve Nyerere alimuongelea mbovu kwenye mahojiano aliyofanya, ila kwa sasa anamtia nguvu kwa wakati huu mgumu anaopitia baada ya kushindwa kwenye kura za maoni ya kuwania Ubunge wa Jimbo la Iringa Mjini.

Upande wa kushoto ni Idris Sultan, kulia Steve Nyerere

Kupitia post aliyoweka kwenye mtandao wa kijamii wa Twitter Idris Sultan ameandika kuwa, "Sitaki kuwa mnafki, kaka Steve juzi kaniongelea mbovu sana kwenye interview, mambo ambayo hata kama ni kweli au la angeweza niambia personally, nikahojiwa na mimi nikasema siwezi ongea ni mkubwa wangu tena hasa sasa anavyoutafuta ugali wa chama, Mungu awe nawe kwenye wakati huu mgumu"

Steve Nyerere ameshindwa kwenye kura za maoni kwa kupata kura 6 ambapo mshindi ni Jesca Msambatavangu aliyepata kura 190, ambapo jimbo hilo lilikuwa na jumla ya watia nia 57.