Tamko la Basata kwa wasanii wanaogombea Ubunge 

Jumamosi , 27th Jun , 2020

Baraza la Sana la Taifa (BASATA) wamesema hawana tatizo na wasanii wote wanaogombea Ubunge kwani ni moja wapo ya fursa na wanataka waichangamkie vyema ili waweze kuwa Wabunge.

Kulia ni msanii Mwana Fa, kushoto ni Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA)

Akizungumzia hilo Katibu Mtendaji wa Basata  Godfrey Mngereza ameeleza kuwa  "Wasanii wachangamkie fursa ya kuwa Wabunge, wapo wasanii wengi ambao wapo Bungeni kama Prof Jay na Joseph Mbilinyi "Mr II Sugu", msanii atakayezungumzia changamoto za wasanii kwenye muhimili wa Bunge ndiyo msanii tena nitapata faraja kweli, katika hili Basata tunawapongeza sana wasanii ambao wanaonyesha nia katika kugombea uongozi ni haki yao ya msingi

Mpaka sasa wasanii waliotangaza nia ya kutaka kugombea Ubunge kwenye uchaguzi mwaka huu 2020 ni Mwana Fa (Muheza,Tanga), Shilole (Igunga Tabora), Baba Levo (Kigoma Mjini), Steve Nyerere (Iringa Mjini) na Wakazi (Ukonga, Dar Es Salaam).

Zaidi tazama kwenye video hapa chini.