Jumatano , 3rd Sep , 2014

Mwanamuziki mkongwe wa miondoko ya Afro Pop nchini Zimbabwe Oliver Mtukudzi amewashtua mashabiki baada ya kuweka wazi kuwa hatoshiriki kwenye tuzo za muziki zijulikanazo kama Zimbabwe Music Awards ambazo zitafanyika mwaka huu.

mwanamuziki wa Afro Pop nchini Zimbabwe Oliver Mtukudzi

Tuku ameelezea kuwa sababu ya yeye kutoshiriki katika tuzo hizo ni kuwa imefika wakati wa kuwaachia vijana zaidi waweze kutambulika na kujitangaza zaidi kimataifa ili kujitengenezea njia za kuweza kushinda katika soko lililopo.

Aidha Tuku ambaye amewahi shinda tuzo mbalimbali kubwa za kimataifa amewashukuru wadau na mashabiki wote ambao wamekuwa wakimsapoti katika kazi zake na ataendelea kushirikiana nao katika kuinua muziki wa nchini Zimbabwe.