Upande wa Aslay wajibu kuhusu skendo ya ulevi

Jumatano , 15th Mei , 2019

Baada ya Zest kusema hajalipwa baada ya kufanya ngoma 10 kubwa za Aslay, meneja wa msanii huyo Chambuso amesema msanii wake hana tatizo na producer huyo.

Msanii Aslay

Chambuso amepiga stori na eNewz na kuweka wazi kuwa  Zest ni ndugu yao na wameshapanga kukutana na kuongelea malipo hayo.

Chambuso pia ameongelea skendo ya Aslay kutumia pombe kupita kiasi na kusema jambo hilo sio la kweli bali ni namna tu Aslay alivyo mpole na mtulivu kwahiyo watu wakimwona hivyo wanadhani amekulewa.

Zest alitengeneza midundo ya ngoma nyingi za Aslay tangu alipotoka kwenye kundi la Yamoto Band na kuanza kufanya muziki wa solo akianza kutoa ngoma ya 'Angekuona'.

Zaidi tazama hapo chini.