Jumapili , 9th Aug , 2015

Usahili wa mwisho Dance 100% 2015 wakamilika kwa 'mtiti'.

mashindano ya kucheza muziki ya Dance100% 2015

Usahili wa mwisho wa Dance 100% 2015, umekamilishwa hapo jana katika viwanja vya Leaders Club Kinondoni jijini Dar es Salaam, muamko mkubwa wa makundi yapatayo 28 kutoka ndani na nnje ya mkoa yakiongezea ushindani na burudani zaidi katika michuano hiyo.

Makundi mwengine ambayo yameshiriki katika usahili leo ni Best Plan, A Town Dancers kutoka Arusha, Boko Young Talent, The Quest Crew, TNT, Tatanisha, DMX, House of Kinetix, Majokery, Sababisha, The World Of Champions, Makaba Crew, Hamadombe, Mazabe Powder, Snap Boys Crew, Bustani Dancers, TGE Hardware, Best love, Chipukizi Dancers, Danger Boys, Butterfly kutoka Mbeya, Bata Boys na Fresh Crew.

Katika michuano ya jana, Wazawa Crew, The Best, Quality Boys, Majokeri na kundi la wasichana la Cute Babies waliweza kuwashawishi majaji na kuweza kujivunia alama nyingi zaidi zilizowawezesha kushinda nafasi ya kuingia robo Fainali ya Dance 100% 2015.

Kujionea yote yaliyojiri jana, usisahau kutazama shoo ya Dance 100%, Jumamosi saa 12:30 jioni EATV pekee.

Dance 100% 2015 inaletwa kwako na EATV na East Africa Radio na kudhaminiwa na Vodacom Tanzania na Coca Cola, Kinywaji rasmi cha Dance 100% kwa mwaka huu.