Vanessa aelezea yaliyojiri na Jux miezi 9

Jumatano , 10th Jul , 2019

Staa wa kike wa muziki wa Bongofleva hapa nchini Tanzania Vanessa Mdee, aeleza ukweli wote kuhusu kuvunjika kwa mahusiano yake na staa mwenzie Juma Jux.

Vanessa na Jux

Vanessa Mdee amefunguka hayo yote kupitia ukurasa wake wa Instagram, baada ya kuulizwa maswali mengi kupitia LIVE session ya mtandao huo kuhusu yeye na Jux.

"Juma na mimi tumeachana tuna miezi zaidi ya miezi tisa, tumeachana kwa muda mrefu sana, tuliogopa kutangaza kama tumeachana kwa sababu tungeleta madhara kwa watu wengi, isitoshe sisi tunafanya vitu vingi vya biashara'', alisema Vanessa.

Pia aliongeza kuwa wawili hao walikuwa na vitu vingi wanamiliki kwa pamoja, pamoja na kazi nyingi za kufanya na hiyo ndio sababu iliyofanya wasitangaze kwa watu, lakini akasisitiza yeye na Jux ni washkaji na ni watu ambao walikua na mahusiano kwa muda mrefu.

Wiki kadhaa zilizopita Vanessa Mdee, alitangaza kuachana na Jux katika mtandao huo wa Instagram bila kueleza sababu zozote.

Mahusiano yao yalikuwa yanapendwa na kufuatiliwa na watu wengi na walianza mahusiano yao mwaka 2014 na wamefanya kazi pamoja kama nyimbo ya juu, sumaku na ziara ya kimuziki ya in Love & Money.