Alhamisi , 16th Mar , 2017

Aliyekuwa meneja wa Manifongo G Maker amekiri kumtamkia msanii huyo kauli yenye utata huku akieleza kushangazwa na hatua ya msanii huyo kuondoka chini ya mikono yake kimyakimya na kuanza kusimamiwa na aliyekuwa dereva wa msanii huyo.

Manfongo

Akizungumza kwenye kipindi cha eNewz ya EATV, G Maker ameitaja kauli hiyo kuwa ni ile aliyosema amesema  "Aliyepata kapata na aliyekosa kakosa" huku akiweka wazi sababu iliyomfanya Manfongo pamoja na dereve huyo kuondoka, ni wao kushindwa kufuata misingi aliyokuwa amewawekea.

"Mimi nilikuwa nimemkabidhi Wasowiso awe anamuendesha Manfongo kwa kuwa alikuwa bado kwenye kuendesha gari, lakini poa yule ni mtoto wa mjini njia nyingi anazitumia, tulipokuja kushindwana ni pale mimi nilipokuja kuwapa misingi yangu ya kufanya kazi wakashauriana na kuondoka pasipo kunijibu chochote"

G Maker ameongeza kuwa habari za Waso kuwa Meneja wa Manifongo amezisikia na kuziona kwenye vyombo vya habari jinsi msanii huyo akiwa anamtuhumu.

Huyu hapa G maker