Alhamisi , 15th Jun , 2017

Msanii kutoka 'Tip Top Connection' Madee Ali amefunguka kwa kudai amefanya mageuzi katika nyimbo ngumu za Hip hop na matokeo yake sasa hivi watu wamemchukulia kama kioo kwa kufanya kazi zao vizuri.

Madee amebainisha hayo kupitia eNewz ya EATV baada ya kulizwa alikuwa anamaana gani alivyoandika katika mtandao wake wa kijamii kuwa 'wale mliowaamini kuwa ni ma-raper wenu bora siku hizi hawarapu tena' ndipo aliposema 

"Japo watu wanajaribu kuficha ficha lakini kitu kipo wazi huwezi kufanya kazi miaka nenda rudi haupati faida 'so' bila ya kutumia akili ya ziada kufanya mabadiliko ya biashara yako basi, wewe kila siku utakuwa unawasindikiza watu. Ile twitter yangu niliyoandika nilimaanisha kwamba wakati natoa wimbo wa hip hop haiuzi' nilipingwa, nilikoselewa sana na yale makoseleo yote niliyachukua kama 'challenge' tu kwenye maisha yangu ya muziki, nilizichukua lakini wenyewe baadaye nikikaa nao pembeni ya 'mic' wanasema kwamba bwana ni kweli" alisema Madee

Madee amesema 'style' ya ubadilikaji wake wa kuimba muziki umewafanya wasanii wengi nao kubadilika kutoka katika kuimba hip hop ngumu na matokeo yake sasa hivi wanaimba hip hop laini.

"Nadhani hata wao wamenitumia mimi kama kioo, wakagundua kumbe hii iko hivyo ndio maana unaona watu sasa hivi wanalainisha kuanzia 'instrumental', mashairi, melodi na miziki yao inapigwa kwenye klabu pamoja na kwenye radio vipindi vyote kuanzia asubuhi mpaka jioni wakati kipindi kile tulikuwa tunasikia katika vipindi vya mchana tu kwenye zile ngumu nyeusi" alisisitizia Madee

Mtazame hapa anavyofunguka zaidi;