Jumatano , 18th Feb , 2015

Msanii wa muziki Vitalis Maembe, amewataka vijana kufahamu uwezo wao na umuhimu kwa taifa hili kwa kushiriki katika katika mambo makuu matatu yanayolikabili taifa hili, katika mwaka huu ambao pia ni wa uchaguzi mkuu.

Vitalis Maembe

Kauli hii ya Vitalis inakuja kama hamasa kwa Vijana wenye sifa, kuungana na kampeni ya ZamuYako2015 inayoendeshwa na kituo hiki, kuhamasisha vijana kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura, kushiriki kupiga kura ya maoni pamoja na kupiga kura katika uchaguzi mkuu.