Jumanne , 13th Dec , 2016

Kampuni ya mtandao wa simu ya Vodacom Tanzania imewashauri vijana hususani wenye vipaji vya sanaa za muziki na uigizaji kutumia jukwaa la EATV Awards ili kutangaza kazi zao kimataifa.

Mkuu wa Mawasiliano VODACOM, Nandi Mwiyombella (wa pili kushoto) akikabidhi tuzo kwa Alikiba katika usiku wa EATV Awards

Vodacom ambao walikuwa ni miongoni mwa wadhamini wa Tuzo za EATV zilizohitimishwa mwishoni mwa wiki, imesema kuwa imeamua kufanya kazi na EATV kutokana na kuamini kuwa kuna mwanga mbele kwa kuangalia mfano katika mashindano ya Dance100% ambayo pia Vodacom inadhamini.

Akizungumza na EATV na EA Radio Mkuu wa Mawasiliano wa Vodacom, Nandi Mwiyombella ambaye alikuwa ni mmoja kati ya waalikwa wa tukio hilo la utoaji tuzo amesema Vodacom imeridhishwa na jinsi shughuli nzima ilivyopangwa na kufanyika na kwa kiasi kikubwa malengo yao yametimia.

Msikilize hapa

Nandi (Katikati) kwa niaba ya Vodacom, akitangaza rasmi kampuni hiyo kudhamini tuzo za EATV katika uzinduzi uliofanyika mwezi Agosti mwaka huu

 

Tags: