Jumatano , 25th Jun , 2014

Kundi la muziki la Wagosi wa Kaya limeendelea na mashambulizi kupitia ujio wao mpya kabisa ambapo wametengeneza video safi ya ngoma yao inayokwenda kwa jina Taxi Driver.

Wasanii wanaoliunda kundi la Wagosi wa Kaya nchini Tanzania

Kundi hili maarufu lenye maskani yake mkoani Tanga limekuwa mstari wa mbele haswa kwa kuwakumbushia mashabiki wao ladha za zamani katika mtazamo mpya kabisa wa kazi hiyo mpya.

Wasanii hawa pia wana video mpya mbili, Bao pamoja na Gahawa ambazo zote pia zimetoka hivi kabribuni kuashiria kurejea kwa kundi hili na nguvu mpya kabisa.