Jumapili , 24th Dec , 2023

Muigizaji wa filamu Tanzania Nana Dollz ameibuka kuwachana baadhi ya wanaume wanaoendekeza tabia ya uongo baaada ya kutumiwa ujumbe DM na mwanume mmoja akimwambia yupo tayari kulea hata watoto wake 7 hata kama hakuzaa naye.

Picha ya Nana Dollz

“Wanaume ni waongo. Mmoja nimemkuta DM anasema yaani wewe hata ungekua na watoto saba na mimi ningeongeza wa nane niwalee wote” - Ameandika muigizaji Nana Dollz

Nana Dollz kwa sasa ana mtoto mmoja wa kike aitwaye Soraya Dollz aliyempata na Fuego Tz.