
"Moja ya kitu kinafanyika sana kwenye sanaa yetu,ni watu kuonesha picha kubwa ingali ndani vipato vyao ni vidogo,madogo wengi wanakubali kuingia kwenye mifumo ya maisha ambayo sio ya kwao, wenyewe wanasema wanajibrand'' Amesema Touch
"Navyojua brand ni pesa tu ukiwa na pesa brand inakuja yenyewe,kuiga mifumo ya mtu ambaye amefanikiwa huo ni ukichaa hawa watu wanawaficha vitu vingi sana kama hamjui,ndio maana wanawajaza mnavimba halafu mwisho wa siku wanawaachia vituko,kubali kwanza kuishi maisha yako,stress ni ugonjwa wa kizungu kinacho wasumbua wengi ni kiherehere na kutokutaka kupitwa" Amesema Touch
"Kama unataka kujibrand hakikisha balance yako ya bank imetuna, i don't believe fake until you make it sitaki huo ukichaa,unaweza ukafake na mwisho wa siku visije kama unavyodhani wewe,ishi maisha yako usiliishi jina litakuchanganya haya ni makompyuta tu yanatutengeneza,ukitaka kuishi kumpyuta utaishia kuchanganyikiwa tu nothing else" Amesema Touch