Jumamosi , 22nd Aug , 2015

Katika kuelekea hatua nzito ya robo fainali ya mashindano makubwa ya Dance 100% 2015, makundi 15 yaliyofanikiwa kuingia hatua hiyo huku kila mmoja akiwa anajiamini kwa kiasi kikubwa, wameanza kutambiana kuukwaa ushindi wa mashindano hayo mwaka huu.

Washiriki watakaochuana hatua ya Robo Fainali Dance 100% 2015

kupitia eNewz, Makundi mahiri ya Team Ya Shamba, Quality Boys na Wazawa Crew leo hii wameweza kuongea na mashabiki zao Afrika Mashariki kuwaeleza vile walivyojipanga na nia yao hasa ya kuukwaa ushindi wa Dance 100% 2015 wenye zawadi ya kitita cha shilingi milioni 5.

Endelea kutazama eNewz kila siku kupata nafasi ya kutazama makundi yote yaliyoingia katika hatua ya Robo Fainali yakiwa na ujumbe kwa mashabiki wao, na vilevile usikose kutazama show kali ya Dance 100% kila Jumamosi saa 12:30 jioni kufahamu kila hatua na kinachojiri katika Dance 100% 2015.