Wema ashindwa kuzuia hisia zake kwa AliKiba

Jumatano , 1st Mei , 2019

Mwanadada kutoka kiwanda cha filamu nchini, Wema Sepetu amesema kuwa hawezi kuficha hisia zake kwa mwanamuziki wa Bongofleva, Alikiba, kutokana na wimbo wake mpya wa 'Mbio' kuwa mzuri.

AliKiba akiwa na Wema Sepetu

Wema amesema kuwa anapenda kumsifia mtu akiwa anafanya kitu kizuri maana kuficha hisia zako kwa kitu kizuri hiyo inakuwa ni dalili ya roho mbaya ambayo kwa upande wake hataki kuikaribisha roho mbaya kwenye maisha yake ya kila siku.

 “Ni hivi tuelewane Kiba anaimba mimi namkubali sana na ni shabiki wake mkubwa siku zote hivyo kama kuna mtu kavimba anune apasuke mimi sijali kabisa kwani kuna mtu anateseka?", amesema Wema.

Hivi karibuni mwanadada huyo alichapisha video akiimba wimbo mpya wa AliKiba 'Mbio' suala lililoibua mjadala kwenye ukurasa wake huo wa instagram.