Jumapili , 3rd Jan , 2016

Nyota wa muziki wa dansi Christian Bella amezidi kuutendea haki mwaka 2016 ambapo anatarajia kufanya kolabo na kundi la wasanii nyota wa miondoko ya Hip Hop, Weusi.

Nyota wa muziki wa dansi Christian Bella

Bella aka King Of The Best Melody amesema kuwa pamoja na colabo hiyo inayotarajiwa kuachiwa hewani muda wowote kuanzia sasa, hakuacha kuelezea furaha yake ya kuanzisha studio yake binafsi inayotarajiwa kuwa tayari hivi karibuni.