Jumatano , 5th Jul , 2017

Rapper Joh Makini amesema kitendo cha mashabiki  kuanza kutafsiri neno moja moja katika wimbo wa 'Amsha Dude ni  ishara kwamba malengo yao yamefanikiwa  ya muziki kupenya kwa watu tofauti  na umefika sehemu iliyokusudiwa.

Msanii Joh Makini

Joh Makini amefunguka hayo akiwa na wasanii wenzake kutoka kundi la Weusi kwenye, Planet Bongo ya East Africa Radio, ambapo alisema kila mtu mmoja mmoja ana uhuru wa kutafsiri awezavyo na kwamba huo ndio ushindi kwao.

"Mtu mwingine anaweza kuutumia kwa matumizi yake mengine, na wewe unaweza kuutumia kwa matumizi yako mengine lakini the same time wote mnapata burudani na target yetu kubwa ni kuhakikisha muziki unakuwa mkubwa,” Joh Makini alifunguka.

Aidha Msanii  Nikki wa Pili ambaye pia ni msemaji wa kundi hilo amefafanua kuhusu wimbo huo na kusema kuwa  “Ujumbe ni kwamba amsha dude katika lolote unalolifanya, kama unatangaza usikwepeshe, amsha dude, kama unafanya mixing, amsha dude, na kama una ndoa amsha dude”.

Wakati huo huo wanachama wa kundi hilo wametoa 'hits' mfululizo kwa kipindi kifupi kama Quality time ya Nikki wa Pili na G nako, Nuru pamoja na Lucky Me za G Nako, Ya Kulevya na Amsha Dude walizoimba wote kwa pamoja.