Msanii wa miondoko ya bongofleva Witnesz Mwaijaga
Witnesz ameongea na eNewz kuwa kati ya video hizo mbili alizoachia hii leo kupitia EATV mojawapo ni yake binafsi aliyoibatiza jina 'Chunga Mdomo Wako' huku ya pili ambayo ni ya mpenzi wake Ochu Sheggy iliyobatizwa jina 'Ntendezeze'.
Witnesz amesema kuwa sababu ya kurelease pamoja video hizo mbili ni kama jibu tu la walio wengi waliotokea kuchanganyikiwa na kudhani kuwa wawili hao wamekuwa pamoja kama kundi, baada ya awali kutoa track mbili za pamoja zikiwemo 'Zaga Zaga' na 'Think About It' ambazo ni project za Otchunes zikiwa ni muunganiko wa majina Ochu Sheggy na Witnesz.






