Alhamisi , 16th Dec , 2021

Baby Mama wa Diamond Platnumz na mfanyabishara Zari The Bosslady amekuwa mwanamke wa kwanza Afrika Mashariki kufikisha followers milioni 10 kwenye mtandao wa Instagram.

Picha ya Zari The Bosslady

Mzaliwa huyo wa Taifa la Uganda anawashukuru mashabiki zake kwa kufikisha idadi hiyo maana sio suala dogo.

"Napenda kuchukua nafasi hii ya kipekee kabisa kuwashukuru vipenzi vyangu wote bila kuwasahau visokolokwinyo maana wao ndio wamejazana hapa kwenye milioni 10, utasema nina serve biriani la Sele Bonge".

"Jamani milioni 10 si mchezo, nasema asanteni sana haya si mapenzi bali ni mahaba ya hali ya juu kabisa nawapenda sana ". ameandika Zari The Bosslady 

Zaidi sikia hapa akizungumzia hilo.