Gabo aiponda 'Bongo Movie' ya sasa

Jumatano , 2nd Nov , 2016

Msanii wa filamu Gabo Zigamba amesema sanaa ya sasa siyo kama ya zamani, na kuna utofauti mkubwa kati ya zama hizo mbili

Gabo Zigamba akiwa Kikaangoni

 

Akijibu maswali ya wananchi kupitia kipindi cha #KIKAANGONI kupitia ukurasa wa facebook wa East Africa Television, Gabo Zigamba amesema sanaa ya sasa ina ujanja ujanja mwingi ingawa inalipa tofauti na ya zamani.

“Sanaa ya zamani ilikuwa ya ukweli lakini haikuwa na maslahi, sanaa ya sasa imekuwa kama ya ujanja ujanja lakini ina maslahi, kwa hiyo sasa hivi tunaweza kuingiza pesa nyingi tofauti na zamani”, alisema Gabo.

Gabo ambaye alijipatia umaarufu mkubwa kwa kuigiza kwenye lafudhi ya Kimakonde, amesema pamoja na umaarufu alionao, hajajutia kuwa maarufu kwani ameweza kutumia fursa hiyo kujitengenezea pesa zaidi, tofauti na baadhi ya wasanii ambao wamekuwa wakisema wanajuta kupata umaarufu, kwani unawanyima uhuru wa kufanya baadhi ya mambo.