Kwa mambo haya, Belle 9 hawezi kumsahau Triss

Ijumaa , 13th Jan , 2017

Msanii wa muziki wa bongo fleva Belle 9 kupitia kipindi cha Kikaangoni kilichofanyika siku ya Jumatano kupitia ukurasa wa facebook wa EATV, amefunguka na kusema hawezi kumsahau producer Triss ambaye ndiye aliyemtengenezea ngoma yake Sumu ya Penz.

Belle 9 (Kushoto) Triss (Kulia)

Belle 9 amesema licha ya maisha ya muziki Triss amemsaidia mambo mengi sana ikiwemo kumfundisha namna nzuri ya kutamka maneno hata kumkumbusha katika mambo mbalimbali pindi anapochepuka kwenye mstari.

"Huwa napenda watu wajue namna gani producer Triss amekuwa msaada kwangu kwenye muziki hata nje ya maisha ya muziki, Triss ndiye mtu aliyekuwa akinifundisha namna nzuri ya kutamka maneno licha ya kuwa nilikuwa naona kwa watu wengine lakini msisitizo mkubwa nilikuwa napata kwake, Triss hata pale alipoona imani yangu kidini inapungua alinisisitiza kwenda kanisani sana. Hivyo amenisaidia mambo mengi sana hata nje ya muziki na hiki kitu napenda watanzania wajue" alisema Belle 9.

Producer Triss