Makonda asimulia alichofanyiwa na Dkt. Mengi

Ijumaa , 12th Apr , 2019

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amesema kwamba Mwenyekiti wa IPP, Dkt. Reginald Mengi aliwahi kumchangia ada wakati akiwa chuoni, na ndiye tajiri pekee ambaye amewahi kufika chumbani kwake kwenye Chuo alichokua akisoma.

Ameyasema hayo leo kwenye sherehe ya kuwatunza askari waliofanya vizuri kwa Mwaka 2018, akisisitiza kuwa katika kipindi hicho hakuwahi kuwa na ndoto ya kuja kuwa kiongozi.

Paul Makonda pia ameyaomba makampuni ya IPP kuunga mkono Serengeti boys, ili kuweza kutoa hamasa zaidi wa mashabiki ili timu iweze kufuzu mashindano yajayo.

Makonda anasimulia zaidi

 

“Tena wakati huo hata ndoto ya kuja kuwa Mkuu wa Wilaya, Kiongozi Vyuo Vikuu haikuwepo, kwasababu wewe ni mlezi wa hii timu tuunganishe nguvu tuingie Brazil”, amesema Paul Makonda.

Hii leo Jeshi la Polisi limetoa tuzo maalum kwa askari ambao wamefanya vizuri kwa mwaka 2018, tukio ambalo lilihudhuriwa na watu mbali mbali ikiwemo wasanii.

Mzee Meni akiwa na Paul Makonda